Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Iraq imeazisha leo mashambulizi ya kwanza ya angani katika ngome za magaidi wa Daesh wanaoungwa mkono na Saudia arabia ndani ya Syria, ikiwa ni hatua ya kulipiza kisasi mashambulizi makali ya karibuni ya kundi hilo mjini Baghdad. Jeshi limesema mashambulizi ya leo yalilenga vituo vya kundi la kigaidi la Daesh katika eneo moja la Syria kwenye mpaka na Iraq. Waziri mkuu Haider al Abadi amesema aliamuru kufanyika mashambulizi hayo. Wiki iliyopita, karibu watu 54 waliuawa katika shambulizi la bomu la kutegwa ndani ya gari lililodaiwa kufanywa na wapiganaji wa kundi la kigaidi la Daesh linalodhaminiwa na Saudia arabia katika eneo linalokaliwa na Waislamu wa dhehebu la shia mjini Baghdad.Wakati huo huo, wanajeshi wa Iraq wameingia katika kitongoji cha magharibi mwa Mosul kwa mara ya kwanza tangu kuanzishwa kwa operesheni kubwa mwezi Oktoba ya kuukomboa mji huo kutoka kwa magaidi wa Daesh. Mapema leo, wanajeshi wa serikali waliukomboa uwanja wa ndege pamoja na kambi moja ya kijeshi mjini humo.
Mwisho wa habari/ 291